Hadithi ya Neema Kitabu cha Wanafunzi Revised

Similar documents
PSC Paper No.19 MUSIC AND SONG IN PR03ECT SUPPORT COMMUNICATION CAMPAIGNS. compiled by Greg tanning Assistant PSC Officer, UNfCEF Nairobi

Paper. A Shaba Swahili life history: Text, translation, and comments

KENYAN LITERARY KISW AHILI 1

African Humanities and the Arts. Series Editor: Kenneth Harrow

My day (part one) /mai dei paat wān Phillip Jones: I'm a businessman. My company sells telephones. filip /aim a biznisman mai kāmpani selz telifounz/

A SHABA SW AHILI LIFE IDSTORY: TEXT AND TRANSLATION

Full terms and conditions of use:

The Pragmatics of Kiswahili Literary Political Discourse

KISWAHILI MEDICALLY. Indiana

AN ANALYSIS OF TRANSLATION CHALLENGES IN THE KISWAHILI VERSION OF SHUJAA OKONKWO

Chapter 1 - Swahili Spelling and Pronunciation

tuuri$ zcat books-all.gz egrep '<GAM>' kw-alg ' mwalimu ' > results

Humor in Kenyan comedy

Jifunze Kiingereza Book Project from Hearts in Unity

Wisdom from Orma, Kenya Proverbs and Wise Sayings

60,000 50,000 THE ABOVE RATES EXCLUDE VAT 18%

Discursive Structure of Humour in Stand-up Comedy Kenya: Discourse Topics and Stylistic Devices in Churchill s Performances

MCHONGOANO AND THE ETHNOGRAPHY OF COMMUNICATION. Claudius Patrick KIHARA Heinrich-Heine-Universität, Düsseldorf

31 st SWAHILI COLLOQUIUM Iwalewahaus, Bayreuth 11 th to 13 th May Programme

Chapter 4 Individuals in East African Musical Worlds Gideon Mdegella and Centurio Balikoowa

Oral Performance and the Creative Imagination in Penina (Mlama) Muhando's Nguzo Mama1

Missing Guards Are Called Unsafe

Wahariri / Editors: Claudia Dal Bianco and Johanna Emig DIWANI YA METHALI AN ANTHOLOGY OF PROVERBS IN KISWAHILI

Beyond Literal Translation. Michael Gichangi Nginye

DOWNLOAD OR READ : MATATU PDF EBOOK EPUB MOBI

THE SWAIDLI MANUSCRIPTS PROJECT AT SOAS

Scholars Journal of Arts, Humanities and Social Sciences

Amedzro (dzrovi) metsoa ame kuku fe tagbç o. (a) Literal Translation: 'A stranger does not hold the head of a coffin.'

Collected and compiled by: Joseph Kariuki Privately published -- Nairobi, Kenya Reviewed by: Angela Taiyana. Nairobi, Kenya May 4, 2007

Golden Musical Memories

Mafumbo: Considering the Functions of Metaphorical Speech in Swahili Contexts

What s the Word? Read!

STCD

IT WAS ALL GLITZ AND GLAMOUR AT THE 2014 KALASHA GALA EVENT KALASHA AWARDS 2014 SPECIAL BULLETIN

Changing Trends in the Form of the Metaphor in Kiswahili Literature

Understanding English Grammar: A Linguistic Introduction

Songs from 34 th Annual National Black Storytelling Festival and Conference. Songs to Share. Song Swap with Ilene Evans and Kwanza Brewer

KNOWLEDGE AND INTELLECTUAL PRACTICE IN A SWAHILI CONTEXT: WISDOM AND THE SOCIAL DIMENSIONS OF KNOWLEDGE

Evolutionary Changes in Thematic Lyrics in Songs with Reference to the Akamba Circumcision Songs in Kenya

The New PSDN Hegemony

A Stylistic Analysis of the Epic of Job

Between innovation & incompetence

Planning for KS2

The Keene Middle School Choir presents. Amy St. Louis, director

David Amunga profile of a music maestro

To Link this Article:

Using Media to scale out Financial Capability in East Africa

You may need to log in to JSTOR to access the linked references.

Contents Preface...4. Fifth Grade...57 Jambo, Jambo!...58 Percussion Concussion II...60 Here Comes the Rain Merrily We Roll Along...

CURRICULUM VITAE. HENRY NAMSYULE WANJALA, PhD. Personal Information: Summary of Expertise. Summary of working Experience

promoting the in your public library

The Nyanga/Ngororombe panpipe dance (double article) 1. THUNGA LA NGOROROMBE THE PANPIPE DANCE GROUP OF SAKHA BULAUNDI

VANESSAMDEE. January 2015

Can Nollywood change financial behavior? An impact evaluation of the Nigerian movie: The Story of Gold

Maisha (which means 'life' in Kiswahili) is a non-profit training initiative for emerging filmmakers in East Africa. (Uganda, Kenya, Rwanda, and

AUDITIONS. Woodland Theatre Presents

Si Clauses French If-Then Clauses

Composition Processes in Popular Church Music in Dar Es Salaam, Tanzania

1 % %.5ƫ+*ƫ0.% 00 '/ƫ0+ƫ%*0!*/%"5 /0+.)ƫ%*ƫ 1 %(!!ƫ EV\Z - E#

OPENING STATEMENT BY HON. DR. HASSAN WARIO, EGH, KENYA S MINISTER OF SPORTS, CULTURE AND THE ARTS KICC, NAIROBI, FRIDAY SEPTEMBER 15,2017

Maduusa-Mata. Big Book Gumuz. Grade 1 Unit 9

RESONATION. Muziki wa Dansi in Dar es Salaam, Tanzania. Nils von der Assen

Dreaming. By Diana Burbano. Oct

We re All here From Around the World Track List

REDEFINING TAARAB IN RELATION TO LOCAL AND GLOBAL INFLUENCES*

KSU Men s Ensemble and Chamber Singers

International Journal of Education and Research Vol. 2 No. 1 January 2014 INCONGRUITY IN STEREOTYPE JOKES BY THE GIKUYU TOWARDS THE GIKUYU

In Need of Connection: Reflections on Youth and the Translation of Film in Tanzania

HYMNS OF THE WABVUWI

Welcome Message 5. Carnival Parade 7. Artists A-Z 9. Festival Timetable - At A Glance 32. Busara Xtra 34. Festival Finalé Party 37

National Anthem - Aboriginal Phonetic lyrics

AUDIENCE CONSUMER TRENDS SURVEY REPORT

LITTLE STONES EDUCATIONAL TOOLKIT LESSON TWO ART. identity? LEARNING OBJECTIVES

Meters and Motion - It s all about the Rhythm!

OFFICE OF SPECIFIC CLAIMS & RESEARCH WINTERBURN, ALBERTA

SINGING TOGETHER today's the day we've been waiting for, - today's the best day of the year. tonight's the night we've been dreaming of.

Available through a partnership with

KWATANCE ONLINE GRAMMAR GRAMMAR TOPICS

Taarab. Shades of Benga

Benefactive, adversative, beneficiary, benefit, adversity, benefactive receptive, adversative receptive, benefactive adoptive, adversative adoptive.

RESEARCH REPORT INTO BOOK DEVELOPMENT INTERNATIONALLY OCTOBER 2008 DRAFT 1

BBC Learning English Words in the News 24 th July 2009 East Africa gets high-speed internet

LUBUMBASHI AND MAYOTTE: TWO RECENT EDITIONS OF SWAHILI-WRITTEN CHRONICLES

The Worship Drum Book: Concepts To Empower Excellence (Worship Musician Presents) By Carl Albrecht

Press Release 20 February 2014

Am I Small? Mimi Ni Mdogo?: Children's Picture Book English-Swahili (Bilingual Edition) (World Children's Book 41) Ebook

Miyambi ya m Chichewa Old Wisdom for New Realities By Montie Mlachila

Copying is illegal. Review copy only. U j œ. œ œ œ œ œ. œ œ. # œ œ œ œ œ œ œ. ? b. œ œ œ œ œ œ œ œ. œ œ. Nancy M. Raabe

KICC, NAIROBI, KENYA. Amalgamating the future of sound, video & light.

January 13, 2008 FREE WITH THE SUNDAY NATION CAN THEY STAND THE 2008 HEAT? PLUS: CENTRESTAGE HARDBALL HEAT

Talking about yourself Using the pronouns je and tu. I can give several details about myself and describe a person s personality.

Tribe of Doris Main Event 2015 Programme by Day

When Kenyan musician Juma Bhalo passed away in April 2014 at the age of seventy- two, his loss

On Migritude Part 1; When Saris Speak The Mother

I really do be[g]-lieve, I really do be[d]-lieve there's joy some[g]-where[c]

Ojibwe, Potawatomi, and Menominee Words. July 20, 2017 College of Menominee Nation Keshena, WI

Fod! By Cristi Cary Miller

ESV Large Print Value Thinline Bible (TruTone, Tan, Ornament Design) By ESV Bibles Crossway READ ONLINE

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION. Instructions

Centering the Peripheral: A Case for Poetry in Africa

Transcription:

Hadithi ya Neema Kitabu cha Wanafunzi Revised 07.02.08 Bible Translation and Literacy Project Mbeya and Iringa Regions P. O BOX 6359, Mbeya Tanzania 2006 44 1

Language: Swahili as spoken in Tanzania Title in English: Kande s Story, Student Book Translated by Joseph Sajine and Julius Msafiri Illustrations by MBANJI Bawe Ernest. This book was translated and produced during workshops held at Nairobi, Kenya, May 29-June 9 and 9 19 October, 2006 Text from Kande s Story, Facilitator s Manual 2005 SIL Africa Area Original Kande stories and illustrations, Books 1-5 2004 Shellbook Publishing Systems (www.shellbook.com) Used with permission. Printing Funded by Ecumenical HIV/AIDS Initiative in Africa Programme of the World Council of Churches 2006 SIL Tanzania 2 43 revised 07.02.08

Somo la 1 Siri ya Mama Neema na Yusufu wakaoana, na baadaye wakapata mtoto. Siku moja familia yao kubwa ilikusanyika chini ya mti alioupenda sana Neema. Nilipenda kukaa hapa na kuzungumza na mama, alisema Neema. Tabu, aliyekuwa mdogo sana wakati wazazi wake wanafariki akasema, Nimewakosa baba na mama, lakini nafikiri wangelijivunia sisi muda huu. 42 3

Siku moja Neema alikuwa ameketi chini ya mti akisoma kitabu. Mdogo wake aitwaye Upendo alikuwa akikimbia akimwita, Neema, Neema! Nimesikia wanawake fulani wakisema, mama anayo siri! Itakuwa siri gani? Neema akasema, Nami nimesikia maneno hayo, nafikiri ninaijua siri hiyo mdogo wangu. Tena akasema, Tukimbie twende kwa mama tukamuulize. Neema na Yusufu walisaidia kuwaalika watu kuja kwenye semina na kuhakikisha wawezeshaji wanapata mahitaji yao. Walifanya juhudi kuwaalika wavulana. Baadhi ya wavulana wanafikiri kwamba kuwa mwanaume kamili, lazima wafanye mapenzi. Yusufu akawaambia wavulana kwamba yeye na Neema wameahidi kuwa hawatafanya mapenzi mpaka pale watakapooana na kuwa waaminifu kwa kila mmoja wao. 4 41

Ana akaanza kuchora picha na kutafsiri masomo kwa lugha yake, ili wawezeshaji watumie kuwafundishia watu kwenye semina. Alitengeneza vijitabu kwa lugha yake vilivyohusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na pia vilihusu jinsi gani ya kuwatunza watu walioathirika na UKIMWI. Neema na Upendo walifika nyumbani wakipiga kelele na kuhema sana. Ndipo Ana, Tabu na kaka yao Petro wakafika wakakusanyika mbele yao ili waone kitu gani kimewafurahisha. Mama yao akawaambia, Nyamazeni ili baba yenu apate muda wa kulala. Akaenda nao mbali kidogo. Upendo akamwuliza mama, Je unayo siri? Mama akashika tumbo lake akajibu akasema, Familia yetu inaongezeka kuwa kubwa zaidi. 40 5

Kisha Tabu aliyekuwa na miaka minne akasema, Ninakwenda kumwambia baba. Kabla hajafika mlangoni mama akamshika akamwambia Tabu, Mwache baba yako apumzike kwa sababu anaijua siri. Tabu hakupenda hali hiyo. Alipenda sana kucheza na baba yake kama ilivyokuwa kawaida yake. Na kwa wakati huo hakuruhusiwa kwenda karibu na baba yake, ambaye muda wote alikuwa akilala, na hafanyi kazi yoyote. Baba alikuwa mnyonge, dhaifu na aliyekonda sana. Familia yote ilimjali sana baba yao. Upendo akaanza mara moja kufundisha semina. Kwa nguvu zake na ucheshi wake aliwafanya watu wamsikilize kwa bidii kuhusu madhara ya UKIMWI. Kwa muda mfupi akawa mwezeshaji mzuri katika jamii yake na watu wengi wakawa wanahudhuria semina zake. 6 39

Mmoja wa waandaaji wa kongamano hilo alimkaribia Neema, akamwambia, Tunataka wewe, Upendo na Ana muwasaidie watu kuwafundisha jinsi ya kujikinga na UKIMWI. Kwa sababu ninyi mna uzoefu na mnajua umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya UKIMWI kuliko mtu mwingine awaye yote. Tena wote mnasoma vizuri sana. Hata watu wanajua kuwa mnajua vizuri ukweli kuhusu virusi vya UKIMWI. Wote wakakubali kwa furaha sana. 38 Siku moja Neema alikuwa sokoni, akamwambia rafiki yake kuwa mama yake anatarajia kupata mtoto. Ndipo mvulana mmoja aliyekuwa anapita pale aliposikia akamdhihaki Neema akisema, Inawezekana mtoto akazaliwa na virusi vya UKIMWI kwa sababu baba yake ana UKIMWI. Neema alikuwa hajui yule mvulana anamaanisha nini. Ndipo Neema akajifikiria akasema, Hakika baba hana UKIMWI au inawezekana anao? Marafiki zake Neema wakamtia moyo wakisema, Usimsikilize mvulana huyo. 7

Ilipofika jioni Neema akamwuliza mama yake akasema, Je baba ana virusi vya UKIMWI? Naomba unieleze mama, mimi ni mtu mkubwa sasa ni lazima nijue. Mama akatazama upande mwingine. Neema akamtazama mamaye akamwona analia. Mama akamjibu Neema akisema, Ndiyo. Samahani mwanangu kwa sababu umesikia habari hizi kwa watu wengine kwanza. Je, tutafanya nini baba akifa? Neema aliuliza Na mahitaji yetu tutapata wapi? Mama akamjibu Neema akasema, Mungu atatusaidia. Ndipo wakalia pamoja kwa kitambo. 8 Mara baada ya hayo, kanisa lilifanya kongamano kuhusu njia za kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI. Wawezeshaji na wanaojifunza walikuja kutoka maeneo yote. Neema, Upendo na Ana walihudhuria. Walimleta hata kaka yao Petro. Na Yusufu naye alihudhuria pia. 37

Siku moja, baada ya mwaka kupita, Neema alimwambia Yusufu akasema, Watu wa kanisa wametusaidia kwa kiwango kikubwa sana! Wametupa shamba lao, nasi tumepanda mazao. Wametufundisha kuwa na maisha mazuri, na wamekuwa marafiki kwa njia nyingi sana. Je, tutawalipa nini kwa yote hayo mazuri waliyotufanyia? Baba yake Neema alikufa kabla ya majira ya mvua kuanza. Rafiki na ndugu wengine walikuja kuomboleza nyumbani kwao. Neema alikuwa anajiuliza kuwa, Kwa nini wanakuja sasa kututembelea hali wakati baba alikuwa mgonjwa na mpweke sana hawakuonekana? Kiongozi wa kanisa tu ndiye alikuwa anaonekana hapa, alionyesha wema. 36 9

Somo la 5 Jamii ya Akina Neema Yajifunza Kuhusu UKIMWI Baada ya msiba kuisha, siku moja Neema na mama yake walikuwa wanaokota kuni porini. Neema akamshika mama yake mkono, wakakaa chini ya mti wakapumzika kwa kitambo. Hali ya mama yake ilikuwa ya udhaifu sana na alionyesha kupumua kwa shida. Mama akamwambia, Binti yangu Neema mimi siwezi kufanya kazi yoyote na kwa wakati wowote. 10 35

Somo la 2 Matatizo Yanaongezeka katika Familia ya Neema Neema alikuwa na furaha kwa vile Yusufu alimsaidia mara kwa mara kufanya kazi shambani wakati watoto wanacheza pamoja. Neema akamwambia Yusufu, Wakati wazazi wangu wamefariki, nilifikiria kuwa familia yetu ingekufa pia. Maisha bado ni magumu, lakini sasa tuna matumaini ya baadaye. 34 11

Neema na mama yake walikuwa wameketi chini ya mti, mama yake alikuwa dhaifu na mgonjwa sana, ilimbidi Neema amsaidie kumnyanyua. Neema na familia nzima, hata Tabu, walifanya kazi katika shamba lao jipya walilopewa na kanisa. Upendo na Ana walijifunza kushona, kanisa liliwaruhusu kutumia vyerahani. Petro alijifunza kazi ya useremala kwenye kituo cha kanisa. Neema akaanza kwenda kwenye mikutano ya kanisa na wadogo zake. Mara wote wakaamua kuchagua njia mpya ya kuishi, jinsi walivyojifunza kanisani. 12 33

Siku moja yule ndugu yao alituma ujumbe kwa Neema. Akasema kwamba sasa ni wakati mwafaka wa Neema na wadogo zake kuondoka katika nyumba ya baba yao na kuacha hata shamba. Neema na wadogo zake wakahuzunika sana. Mwanamke mmoja kutoka kanisani aliwakaribisha kuja nyumbani kwake, wakaanza kuishi pale. Na alikuwa anawasaidia hata kipindi mama yao alipokuwa mgonjwa. Alikuwa anaishi karibu na kanisa na lile shamba pia. Watoto wakaondoka kwenda kuishi naye, na ndugu yao akachukua nyumba na shamba lao. 32 Baba yake Neema alifariki, na mama yake mjamzito alikuwa dhaifu sana, Neema pamoja na wadogo zake ilibidi waongeze bidii katika kazi zao za nyumbani. Neema alikuwa anawakaripia wadogo zake, wakati akifikiria kuwa hawafanyi kazi kwa bidii kama inavyotakiwa. Hivyo mama yake akamgombeza akisema, Mimi ningali bado mama wa familia hii. 13

Ndipo wanawake wawili kutoka kanisani wakafika nyumbani kwao kuwatembelea. Moja wao alikuwa mfanya kazi wa idara ya afya, na mwingine alikuwa msimuliaji hodari wa hadithi. Walifanya kazi nyingi za akina mama. Walikuwa wanaleta chakula. Walianza kufika mara kwa mara. Walikuwa wakisimulia hadithi. Neema alifurahi sana alipoona mama yake akicheka mara kwa mara. Baada ya wadogo zake kurudi na kumweleza kuhusu shamba la jumuiya ya kanisa, Neema akaamua kujihusisha. Viongozi wa kanisa waliwaruhusu kulima sehemu kubwa ya shamba, na waliruhusiwa kutunza chakula au kuuza sokoni pale inapobidi. Ndipo wakaanza kufanya kazi kwa bidii sana, maisha yao yakawa bora kuliko yalivyokuwa mwanzoni. Upendo aliweza kurudi tena shuleni, akaendelea na masomo. 14 31

Yusufu aliendelea kumwomba Neema mpaka siku moja Ana mdogo wake neema alisema, Nami leo nitakwenda kanisani. Labda ninaweza kujifunza kitu chochote. Naye Upendo alisema, Nami leo nitakwenda pia. Labda nitapata marafiki wengine. Ndipo Neema akasema, Wachukue Tabu na Yatima muondoke nao. Petro na mimi tutakaa hapa nyumbani kufanya kazi zilizosalia. 30 Neema alimsikia mhudumu wa afya akizungumza na mama yake. Lakini hakuelewa vizuri kila kitu kilichokuwa kinaongelewa, ndipo akajifunza kwamba baba yake hakuwa mwaminifu kwa mama yake. Labda baba aliambukizwa virusi vya UKIMWI na mwanamke mwingine. Baba hakuelewa kwamba ana virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo hakufanya kitu chochote kumlinda mama. Inawezekana mama aliambukizwa na baba virusi vya UKIMWI, na mtoto naye angeweza kuambukizwa virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama. Lazima ufike kliniki kupima kama una virusi vya UKIMWI, Mhudumu wa afya alimwambia mama. 15

Mama alikwenda kliniki. Muuguzi alichukua damu kutoka mkononi mwa mama. Hakujisikia maumivu, muda si mrefu mama akapata matokeo ya kipimo cha damu yake. Siku iliyofuata mama alimwambia Neema habari za kusikitisha. Mama alikuwa ameambukizwa na virusi vya UKIMWI. Mtoto angeweza kuwa ameambukizwa pia. Baadaye kule kliniki, mhudumu alimpa mama yake Neema madawa ya kutibu magonjwa nyemelezi ambayo yanasaidia kuwapatia nguvu watu wenye virusi vya UKIMWI. Lakini madawa ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI yalikuwa hayapatikani katika jamii yao. Mama alikuwa na wasiwasi kuhusu mtoto wake, kuwa ni wapi angeweza kupata madawa yanayohitajika kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa mtoto atakayezaliwa. 16 Mvulana mmoja kutoka kijijini kwao jina lake aliitwa Yusufu, mara nyingi alikuwa anamtembelea Neema. Alikuwa anakwenda na mdogo wake mchanga, alikuwa anamwambia Neema, Twende wote kanisani. Siyo muda huu, Neema alikuwa anamjibu yule mvulana hivi, Nina kazi nyingi sana za kufanya. 29

Neema na wadogo zake walipita katika kipindi kigumu sana. Wazazi wao walikufa kwa UKIMWI, na kuwatunza wadogo zake wote ilikuwa ni kazi ngumu kwake. Mara nyingi walishinda na njaa, lakini Neema alifanya kazi ngumu sana kwa ajili yao, na alijaribu kuwa kama mama kwa Yatima. 28 Hali ya mama ikazidi kuwa mbaya sana. Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yakaongezeka na muda mfupi mama akawa na UKIMWI. Alikuwa na vidonda vingi katika mwili wake. Neema akawauliza wale wanawake waliotoka kanisani, Je, ninaweza kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nikimgusa mama? Yule mhudumu wa afya akamjibu, Huwezi kupata, kama utakuwa mwangalifu. Akamfundisha Neema njia bora na salama kabisa za kumhudumia mama na kumfundisha vyakula bora vya kumpa mama yake. Neema akahakikishiwa kabisa usalama kuwa hawezi kuathirika akimhudumia mama yake. 17

Somo la 4 Neema Anapata Matumaini Mtoto alipozaliwa. Mama akawa dhaifu sana. Akamshika mtoto na kulia akisema, Yatima. Mama akafariki baada ya siku chache na Neema akamwita mtoto jina lake Yatima. Neema akampakata mtoto mkononi mwake na kukaa chini ya mti akasema. Sitakuacha kuwa yatima, utakuwa mtoto wangu sasa. 18 27

Somo la 3 Familia ya Neema Yakabiliwa na hatari. Upendo akawa na wasiwasi kuwa mwanaume aliyempa bangili alikuwa anajaribu kutaka kufanya mapenzi naye. Neema, Upendo na Ana wakaahidi kutofanya mapenzi mpaka watakapoolewa. 26 19

Neema alikaa chini ya mti akimlisha mdogo wake Yatima. Alitamani mtu angelimnyonyesha mtoto, lakini kwa kuwa mama alikufa kwa UKIMWI, watu waliogopa kumnyonyesha kwa hofu ya kuambukizwa Virusi Vya UKIMWI kutoka kwa yule mtoto. Kanisa lilimsaidia Neema kwa kumpa mtoto maziwa na maji safi. Neema alifurahi sana kuona Yatima anaendelea vizuri. 20 Mhudumu wa kituo cha afya akawaambia mtoto anaendelea vizuri. Lakini mnatakiwa kusubiri kwa muda wa miezi kadhaa kabla hajapimwa kama ana virusi vya UKIMWI ama hana. Ndipo akawaeleza Neema na Upendo mambo muhimu waliyopaswa kuyafahamu yahusuyo wasichana na wavulana wa rika lao, akawaambia, Kwa kuwa ninyi ni yatima, kuna wanaume ambao watajaribu kuwapa ninyi chakula na zawadi ili kuwashawishi mfanye nao mapenzi, msidanganyike. Mnaweza kupata Mimba au UKIMWI ama magonjwa mengine ya zinaa yanayosababishwa na kufanya ngono. 25

Asubuhi moja Neema na Upendo walikuwa wakimpeleka mtoto kliniki kwa ajili ya kupimwa. Upendo akanyosha kidole kwa mwanamume mmoja aliyekuwa karibu na soko akasema, Yule ni mwanaume aliyenipa bangili hii. Huenda akatusaidia katika maisha yetu. 24 Mdogo wa kiume wa Neema aitwaye Petro akaja na akamwambia, Nataka kuacha shule kama mlivyoacha wewe na Upendo. Neema akamjibu, Hapana unatakiwa kumaliza shule kwanza. Ndipo unaweza kutusaidia sisi wote, Halafu inawezekana Upendo akarudi tena shuleni. Tena uwapo shuleni jiangalie usishirikiane na wavulana ambao wanatafuta wasichana wafanye nao mapenzi. Unaweza kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa na wasichana hao. Pia ni muhimu usijidunge sindano za madawa ya kulevya unaweza kupata virusi vya UKIMWI kwa kuchangia sindano. Petro akasema kwamba atasoma kwa bidii. Akaahidi kwamba hawezi kutafuta wasichana wala kujidunga sindano. 21

Siku moja ndugu yao Neema akawatambelea, akamwambia Neema akisema, Kwa mila zetu ardhi hii ni mali yangu kwa kuwa baba yenu amekufa. Neema akalia akisema, Lakini hatuna mahali pengine pa kwenda. Ndiyo, lakini hilo mimi halinihusu! akasema ndugu yao. Na baadaye nitaitaka nyumba. Lakini muda huu ninataka nusu ya mazao mliyopanda. Jioni hiyo Ana akamuuliza Neema, Je, itabidi tuondoke? Neema akajibu, Hapana, ndugu yetu amesema tunaweza kubaki kwa muda. Lakini inabidi tumpe nusu ya mazao yetu. Hivyo tutabaki na chakula ambacho hakitatutosha, akalia Ana. Tunatakiwa kufanya kitu kingine ili tuweze kupata chakula cha kutosha na kukidhi mahitaji yetu mengine! 22 23